Gavi nje ya dimba miezi mitano

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:32 PM Sep 25 2025
news
Picha Mtandao
Kiungo wa kati wa Barcelona, Pablo Páez Gavira 'Gavi'.

KIUNGO wa kati wa Barcelona, Gavi atakuwa nje ya uwanja hadi kwa miezi mitano baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti lake la kulia, klabu hiyo ya LaLiga imesema.

Gavi, ambaye alirejea kutoka katika jeraha la goti msimu uliopita, hajacheza tangu Agosti, mwaka huu.

"Mchezaji wa kikosi cha kwanza, Pablo Páez Gavira 'Gavi' amefanyiwa upasuaji wa goti," ilisema taarifa ya Barcelona. 

"Muda wa kurejesha unakadiriwa karibu miezi minne hadi mitano."

Barca awali walitarajia upasuaji ungeepukika.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 hapo awali alikosekana kwa miezi 11 baada ya kuumia wakati akiichezea Hispania mnamo Novemba, mwaka 2023.

Barcelona leo itacheza dhidi ya Real Oviedo, kabla ya kuwakaribisha Real Sociedad hapo Jumapili.

Hiyo sasa inamaanisha, Gavi hatarejea hadi miezi michache ya mwisho ya msimu wa Barcelona na kabla ya Kombe la Dunia la 2026 nchini Marekani, Canada na Mexico.