Slot: Kadi nyekundu ya Ekitike ya kijinga

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:40 PM Sep 25 2025
news
Picha Mtandao
Kocha wa Liverpool, Arne Slot.

KOCHA wa Liverpool, Arne Slot, amesema kadi nyekundu aliyooneshwa, Hugo Ekitike, katika mechi dhidi ya Southampton ilikuwa "isiyohitajika na ya kijinga," na mshambuliaji huyo sasa amesimamishwa kwa mechi dhidi ya Crystal Palace wikendi hii.

Ekitike mwenye umri wa miaka 23 aliingia akitokea benchi na kufunga bao katika ushindi wa magoli 2-1 wa Carabao Cup dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield, lakini alioneshwa kadi ya pili ya njano kwa kuvua jezi yake wakati wa kushangilia.

Mchezaji huyo sasa atakosa mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu pale kwenye Uwanja wa Selhurst Park.

"Haikuwa ya lazima na ya kijinga," alisema Slot katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mechi. 

"Haya ni mambo ya kijinga, kwa sababu unapaswa kudhibiti hisia zako.

“Siku zote ni bora kudhibiti hisia zako. Ikiwa huwezi, fanya kwa njia ambayo haitasababisha kadi ya njano.

"Nilimwambia, kama utafunga katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika dakika ya 87 labda naweza kukuelewa.

"Sijawahi kucheza katika kiwango hiki, lakini nilifunga mabao machache na kama ningefunga bao kama hili, ningegeuka na kumwendea Federico Chiesa na kusema: 'Bao hili linakuhusu wewe, hili halinihusu.' Sio lazima kuvua jezi, maana ni ujinga."

Liverpool pia walipata pigo jingine ambapo mlinzi, Giovanni Leoni, alipata jeraha mwishoni mwa kipindi cha pili. 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 alijiunga na klabu hiyo kutoka Parma msimu wa joto.