Vinícius alisifia bao lake

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:22 PM Sep 25 2025
news
Picha Mtandao
Vinicius Junior mchezaji wa klabu ya Real Madrid.

VINICIUS Júnior amesema bao lake katika ushindi wa magoli 4-1 wa Real Madrid dhidi ya Levante Jumanne, lilikuwa "moja ya mabao bora ambayo nimefunga."

Juhudi za fowadi huyo za dakika ya 28 zilimfanya kufunga bao kwa shuti kali katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Ciutat de Valencia.

Franco Mastantuono aliongeza la pili kabla ya Etta Eyong wa Levante kufunga na Kylian Mbappé akafunga mara mbili na kuifanya Madrid kushinda mechi yake ya sita kwenye Ligi Kuu Hispania msimu huu.

"Luka Modric alinifundisha aina hiyo ya kupiga mashuti," alisema Vinícius akiiambia Real Madrid TV baada ya mchezo. 
"Kwa sasa hayupo, lakini nimefurahishwa sana na mchezo huu, na kwa ushindi huu ... Tutegemee naweza kufunga mabao zaidi kama haya. Ni moja ya mabao bora ambayo nimefunga."

Vinícius ameanza msimu huu akiwa ameachwa mara mbili katika kikosi cha kwanza na kocha Xabi Alonso, na kuonekana kutofurahishwa na kubadilishwa katika ushindi wa Jumamosi dhidi ya Espanyol.

Madrid ndio timu pekee kwenye LaLiga iliyo na rekodi ya asilimia 100 ya kushinda mechi zote tangu kuanza kwa ligi na itacheza dhidi ya Atlético Madrid, Jumamosi.

"Ulinzi, umoja wetu, na kufanya kazi kama timu," alisema Vinícius alipoulizwa sababu za mafanikio hayo ya Madrid hadi sasa. 

"Kama tutaendelea hivi, tunaweza kushinda mechi nyingi sana msimu huu. Sasa tunahitaji kupumzika kidogo, lakini tutegemee tunaweza kushinda Jumamosi dhidi ya Atletico Madrid."