Kocha Mkuu wa Yanga, Romain Folz, amesema timu yake imejipanga kikamilifu kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Wiliete Benguela, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 5 jioni.
Folz amesema ingawa walishinda 3-0 katika mchezo wa kwanza, wanamheshimu mpinzani wao na lengo ni kupata ushindi tena ili kuwafurahisha mashabiki.
Mchezaji wa Yanga, Aziz Andambwile, amesema wachezaji watatekeleza maelekezo ya benchi la ufundi kama walivyofanya kwenye mchezo wa awali, wakiwa na lengo la kusonga mbele katika mashindano.
Kwa upande wa Wiliete Benguela, Kocha Bruno Ferry amesema mchezo utakuwa mgumu, lakini timu yake haitakata tamaa licha ya kupoteza mchezo wa kwanza. Mchezaji Mahalatsi Makudubela ameongeza kuwa malengo yao ni kushinda mchezo huo kwani kila kitu kinawezekana.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED