Dk Mwinyi atunukiwa Tuzo ya Muhamasishaji Bora wa uwekezaji Zanzibar

By Rahma Suleiman , Nipashe
Published at 09:47 AM Jun 18 2025
 Dk Mwinyi atunukiwa Tuzo ya Muhamasishaji Bora wa uwekezaji Zanzibar
Picha: Ikulu Zanzibar
Dk Mwinyi atunukiwa Tuzo ya Muhamasishaji Bora wa uwekezaji Zanzibar

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametunukiwa tuzo ya Muhamasishaji Bora wa Uwekezaji Zanzibar.

Dk. Mwinyi alipokea tuzo hiyo jioni ya jana, Juni 17, 2025, visiwani Zanzibar, katika hafla maalum iliyoandaliwa na Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), kufuatia kongamano la uwekezaji.

Tuzo hiyo imetolewa wakati wa hafla ya chakula cha usiku ikiwa ni sehemu ya Kongamano la Kwanza la Uwekezaji 2025 visiwani Zanzibar.

Kongamano hilo lilizinduliwa rasmi na Dk. Mwinyi Juni 16, 2025, katika eneo la Micheweni, Kisiwani Pemba, likiwa na lengo la kufufua uchumi wa kisiwa hicho.