EWURA yatoa vibali 10 ujenzi vituo vya CNG

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:15 PM May 01 2025
EWURA yatoa vibali 10 ujenzi vituo vya CNG
Picha: Mtandao
EWURA yatoa vibali 10 ujenzi vituo vya CNG

Kufikia Aprili 2025,EWURA ilitoa vibali 10 vya ujenzi wa vituo vya CNG katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro kwa Kampuni za PUMA Energy Tanzania Limited kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikuu (Mother Station) - Tegeta na kituo kidogo (Daughter Station) kwenye kiwanda cha Alliance One - Morogoro; Energo Tanzania Limited - Mikocheni, Victoria Service Station Limited - Kipawa, Rafiki CNG Station – Tabata Relini, Tanzania States Natural Gas Holdings Company Limited - Goba, Puma Energy –91 Mbezi Beach na Puma Energy – Ubungo External, Natenergy – Kigamboni.

 EWURA pia ilitoa kibali cha ujenzi wa kituo cha kupokelea gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG Receiving Facility) kwa kiwanda cha Kinglion - Kibaha. 

Pia, EWURA ilitoa leseni tano (5) za uendeshaji vituo vya CNG kwa kampuni za Tembo Energy - Tabata, TPDC - Mlimani, TAQA Dalbit - Sam Nujoma, Rafiki CNGStation - Tabata na leseni ya usafirishaji wa CNG (CNG Supply License) kwa Kampuni ya Tan Health Limited.
 
Kutokana na ongezeko la ujenzi wa vituo vya CNG, unafuu wa gharama unaopatikana katika matumizi ya gesi asilia kama nishati mbadala ya mafuta katika vyombo vya moto na mwamko mkubwa wa wananchi kutumia CNG, idadi ya watumiaji wa gesi hiyo katika vyombo vya moto inatarajiwa kuendelea kuongezeka kwa kasi.
 

Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/26