Aliekuwa mkuu wa ujasusi Saudia amtaka Trump kuharibu kinu cha chuklia cha Israel

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:41 PM Jul 10 2025
news
Picha Mtandao
Turki al-Faisal, mkuu wa zamani wa ujasusi wa Saudia.

Aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini Saudia Turki al-Faisal ameibua mjadala mitandaoni baada ya kuwashutumu viongozi wa nchi za Magharibi katika misimamo yao dhidi ya Iran, Israel huku akimtaka Rais wa Marekani Donald Trump kushambulia kinu cha nyuklia cha Israel kama ilivyofanya kwa Hehran.

Katika makala yake ambayo imechapishwa kwenye tovuti ya ‘The National news’ Al-Faisal amesema: “Ikiwa tungeishi katika ulimwengu ambamo haki inaenea, tungeona ndege za kivita zbn a Marekani aina ya B-2 zikilenga mabomu kwenye kinu cha Dimona na maeneo mengine ya nyuklia ya Israel.”

Ameongeza, “Israel inamiliki mabomu ya nyuklia, na hivyo kukiuka Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Nyuklia. Haijawahi kutia saini mkataba huo ili kuepuka uangalizi wa IAEA. Hakuna anayekagua vituo vyake vya nyuklia.”

Pia amesema wale wanaohalalisha shambulio la upande mmoja la Israel dhidi ya Iran kwa kutaja wito wa viongozi wa Iran kuiangamiza Israel wanapuuza kauli za Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, tangu alipoingia madarakani mwaka 1996, na wito wake wa mara kwa mara wa kuiangamiza serikali ya Iran.

Al-Faisal amesema kwamba unafiki wa nchi za Magharibi na uungaji mkono wao kwa Israel katika shambulio lake dhidi ya Iran ulitarajiwa. Akidai kuwa mataifa hayo yanailinda Israel katika mashambulizi yake yanayoendelea Palestina.