Mmoja auawa huku nyumba ikiteketeza kisa kuua mende

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:34 PM Oct 21 2025
news
Picha Mtandao
Mende aliyeuawa

POLISI wa Korea Kusini wamesema wanatafuta kibali cha kumkamata mwanamke aliyesababisha moto katika jengo lake la makazi wakati akijaribu kumuua mende kwa kutumia kifaa cha kutengeneza moto kama kifaa cha kuteketezea.

Hayo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, na kwamba tukio hilo lilitokea jana ambako jirani mmoja wa mwanamke huyo alipoteza maisha baada ya kuanguka kutoka ghorofani akiwa katika jaribio lililoshindikana la kutoroka kupitia dirisha baada ya kuzuka moto.

Mwanamke huyo, ambaye yuko katika umri wa miaka 20, aliwaambia polisi kuwa alijaribu kumchoma mende kwa kutumia kiberiti na dawa inayowaka moto, na kuongeza kuwa amewahi kutumia mbinu hiyo hapo awali.

Hata hivyo, katika tukio hilo lililotokea juzi ilielezwa kuwa baadhi ya vitu ndani ya nyumba yake vilishika moto.

Polisi katika jiji la kaskazini la Osan walisema mwanamke huyo anaweza kufunguliwa mashtaka ya kusababisha moto kwa bahati mbaya na kusababisha kifo kwa uzembe.

Vyombe vya habari vya ndani, vilieleza kuwa uchomaji mende kwa kutumia vifaa vya kulipua moto au vinavyotengeneza moto nyumbani imekuwa mbinu mpya ya kuondoa wadudu wa nyumbani, miongoni mwa watu.

Ilielezwa kuwa mwaka 2018, mwanaume mmoja nchini Australia aliteketeza jikoni mwake alipokuwa akijaribu kuwaua mende kwa kutumia kifaa cha kutengeneza moto kutokana na dawa ya kuua wadudu.