Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, inatarajiwa leo Ijumaa Oktoba 24, 2025, kutoa uamuzi kuhusu shauri namba 24514 la mwaka 2025, lililofunguliwa na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi na Cuba, Humphrey Polepole, dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na wenzake.
Kesi hiyo, iliyofunguliwa kwa hati ya “dharura sana” na Wakili Peter Kibatala kwa niaba ya Polepole, inaiomba Mahakama kuamuru Jamhuri kumleta Polepole Mahakamani au kueleza alipo, kufuatia kutoweka kwake katika mazingira ya kutatanisha. Inadaiwa kuwa Polepole alichukuliwa na watu wasiojulikana na tangu wakati huo haijulikani alipo.
Shauri hilo limesikilizwa chini ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Salma Maghimbi, kwa utaratibu wa maandishi, ambapo mawakili wa pande zote mbili waliwasiliana kwa kubadilishana nyaraka za hoja zao kabla ya uamuzi wa leo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED