BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imekusanya tani 6.84 ya dhahabu safi yenye thamani ya dola za Marekani milioni 682.66 na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 10 bora barani Afrika zinazohifadhi dhahabu iliyosafishwa.
Imeelezwa kuwa mpango wa serikali kununua dhahabu ulianza Julai 2024, lakini utekelezaji wake ulianza Oktoba lengo likiwa ni kuwa na dhahabu kama sehemu ya hakiba ya fedha za kigeni.
Hayo yameelezwa leo na Naibu Waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa wakati akifunga mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wachimbaji wadogo yaliyotolewa na Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu.
Pia amebainisha kuwa sheria ya madini ya mwaka 2019 kifungu cha 59 sura ya 123 imeweka wazi kwamba anaetaka kuuza dhahabu nje ya nchi lazima asilimia 20 iuzwe benki kuu.
“Sekta ya madini imeendelea kukua na kuongeza pato la taifa kutoka asilimia 9.1 mwaka 2023/24 hadi kufikia asilimia 10.1 mwaka huu. Pia sekta hii imechangia mfuko mkuu wa serikali Sh. Trilion 1.07 kwa mwaka wa fedha 2024/25,” amesema.
Akizungumzia mafunzo, Dk. Kiruswa amesema yemelenga kutoa ujuzi wa nadharia na vitendo utakaosaidia kuboresha uzalishaji wa madini kuanzia hatua ya utafiti,uchimbaji,uchenjuaji,usalama na afya mahali pa kazi na utumiaji mzuri wa vilipuzi.
“Hizi zote ni hatua za kuunga mkono serikali katika kuleta mabadiliko kwa wachimbaji wadogo, tunatambua kwamba tunafursa kubwa ya kutajirika kupitia shughuli ya madini sekta hii ni sekta tarajiwa katika kutengeneza mabilionea,” amesema Naibu Dk. Kiruswa.
Amesema program ya kuongeza ujuzi ilianza mwaka 2016 na hadi sasa serikali imetoa Sh. Bilioni 111 zilizowanufaisha wanufaika 157,909 hadi juni mwaka huu.
“Kupitia program hii maafunzo ya kukuza ujuzi yanatolewa katika maeneo manne ambaayo ni mafunzo ya uanagenzi, uzoefu kazini, maafunzo ya urasimishaji ujuzi unaopatikana nje ya mfumo rasmi wa elimu na mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi walio katika sekta ya umma na binafsi,” amesema Nchimbi.
Amesema mafunzo hayo yamewajengea uelewa wa kanuni za ualama kazini,maarifa ya uchimbaji bora na endelevu,mbinu za kutafuta masoko na kushiriokiana na taasiis za fedha ili kupata mitaji.
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo Mkoa wa Geita Titus Kabuo, amesema wachimbaji huchimba zaidi kwenda chini na bila kupata ujuzi wa namna gani ya kuchimba na kulinda mashimo ni rahisi kupoteza maisha.
Amesema katika mafunzo hayo wamefundishwa namna ya kutunz akumbukiumbu na namna ya kufanya kazi kwa ufanisi na kujipatia kipato.
Kwa mujibu wa Kabuo serikali ya aqwamu ya sita imefanya kazi kubwa katika sekta ya madini ikiwa ni pamoja na kutoa leseni kwa wachimbaji wadogo na kupunguza tozo zilizokuwa zikimfanya mchimbaji ashindwe kupiga hatua.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED