Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMMA, kimetangaza safu 13 ya Sekretarieti yake huku baadhi ya waliokuwa viongozi kabla ya ujio wa wanachama wapya wakipandishwa na kuhamishiwa nafasi nyingine.
Idara ya Bunge, Halmashauri na Serikali za Mitaa imemteua Kayumbo Kabutali kuwa Mkurugenzi. Idara ya Habari na Uenezi imemteua kuwa Mkurugenzi, huku Ipyana Samson akichaguliwa kuwa Naibu Mkurugenzi.
Idara ya Uchumi, Fedha na Mipango imekabidhiwa kwa Catherine Ruge kama Mkurugenzi, na Stewart Kaking’i kuwa Naibu wake, Idara ya Uchaguzi, Kampeni na Oganaizesheni imemteua Ismail Kangeta kuwa Mkurugenzi, akisaidiwa na Manaibu Wakurugenzi David Chiduo na Mohamed Chiduo.
Idara ya Mahusiano, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inaongozwa na Rahman Rungwe akiwa Mkurugenzi, na Aisha Madoga akiwa Mkurugenzi Msaidizi. Idara ya Itikadi na Mafunzo kwa Umma imekabidhiwa kwa Edward Kinabo kama Mkurugenzi, akisaidiwa na Dorothy Mpatiri kama Naibu, Idara ya Sheria, Katiba na Haki za Binadamu bado haijapata Mkurugenzi, lakini Estae Fulano ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Idara hiyo.
Idara ya Utafiti, Tathmini na Ufuatiliaji inaongozwa na Elia Marwa na Bibiana Benecto kama Naibu Mkurugenzi, Idara ya Ulinzi bado haina Mkurugenzi rasmi na kwa sasa imekaimiwa na Prosper Makonya. Katibu wa Sekretarieti ni Julius Mwita, Mtaalamu wa Mikakati ni Regnald Munisi, Mkuu wa Utawala ni Khadija Mwago, akisaidiwa na Salma Sharifu. Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia ni Magreti Mlekwa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED