Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema Dira 2050 imewekewa ulinzi kwa kupelekwa bunge na kwamba hakuna Rais atakayeweza kwenda kinyume nayo.
Aidha,amesema Dira 2050 itatekelezwa na Marais watatu,na kwa atayaletaka kuibadilisha atatakiwa kupeleka bungeni na kwamba Dira hii imekuwa tofauti kwa kuwa ya 2025 iliishia hatua ya kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri.
Waziri Mkumbo ameyasema hayo leo Julai 8,2025 wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali kuhusu kukamilika kwa Dira 2050 itakayozinduliwa Julai 17,2025 na utekelezaji wake kuanza Julai mosi,2026.
"Rais Samia Suluhu aliipeleka Dira 2050 Bungeni ili kuiwekea ulinzi. Tumeiwekea ulinzi mkubwa kupitia Bunge ili iwe sheria,kwamba Rais akitaka kubadilsiha lazima arudi bungeni.
"Tumeweka ulinzi mkubwa ili yeyote aliyepo madarakani hawezi kuamua kuacha kutekeleza,"amesema.
Kuhusu, umuhimu wa vyombo vya habari, amesema kwenye jamii iliyostaarabika ya maana unaipata kwa makundi maalum mawili ambayo ni walimu na waandishi wa habari,anayedharau vyombo vya habari anakosea sana.
Amesema serikali inathamini uwepo vya vyombo vya habari imara,na kwambahuwezi kuzungumzia uwajibikaji wa serikali bila kuwa na vyombo vya habari.
Prof.Kitila amesema mchakato wa kutengeneza Dira 2050 umepitia hatua 13 ambazo ni kuandaa na kuidhinisha miongozo ya Dira.
Mkakati wa kuandika Dira ulianza Aprili 3,2023, kuunda vyombo vya kutathimini mchakato wa Dira,kufanya tathimini ya utekelezaji wa Dira 2025.
Pia kukusanya maoni ya wananchi na wadau juu ya maudhui gani yaingie kwenye Dira,kujifunza kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Asia na Marekani kwa hatua zilizopigwa.
Alizitaja baadhi ya nchi walizojifunza ni Botswana, Moroco,Mauritius, Afrika Kusini na Kenya.
Kwa Asia wamejifunza Kusini mwa Asia za China,Indonesia,Korea Kusini,Singapore na India,na kwamba kwa Ulaya wamejifunza kidogo kutokana na kwamba historia yao si ya muda mrefu kama nchi zenye historia 1,000.
Hatua nyingine ni uchambuzi,uandishi na uhariri wa tqarifa na kutoa Rasimu ya kwanza ya Dira 2050.
Pia kulinda rasmu ya kwanza ya Dira 2050 ilizinduliwa Desemba 2024,na kuchukua Rasimu kupeleka tena jwa wadau ili kupata maoni ya kihariri.
"Tulikutana na wadau mbalimbali kama waandishi wa habari na vyama vya siasa ili kupata makubaliano ya pamoja.Tulivyokutana na vyama vya siasa tulikubaliana tusibishane juu ya tunakwenda wapi ila tukubaliane tuende huku,Ilani zetu ziakisi tunaenda wapi,"amesema.
Hatua nyingine, kutoa rasimu ya pili ya Dira ya Taifa na kukabidhiwa kwa Waziri Mkuu,Juni 2025 iliidhinishwa na Baraza la Mawaziri na kufuatiwa na Bunge.
Aidha,amesema hatua ya mwisho ni kuutaarifu umma kuwa mchakato wa Dira umekamilika na itajulikana kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza Dira 2050 Tanzania Tuotakayo,na hatua ya mwisho ni Rais Samia Suluhu Hassan kuizundua Julai 17,mwaka huu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED