Dk. Samia: Mbolea ya ruzuku inatolewa Tanzania nzima

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:33 PM Sep 04 2025
Dk. Samia: Mbolea ya ruzuku inatolewa Tanzania nzima

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kutoa ruzuku ya pembejeo za kilimo kwani matokeo ya ruzuku hizo yamekuwa ni makubwa hususani kwa Mkoa wa Mbeya ambako wanazalisha zaidi mazao ya pareto, mahindi, mpunga na maparachichi na asilimia 85 ya wananchi wake ni wakulima.