SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limeshinda tuzo kwenye maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF) katika kipengele cha Taasisi za Serikali.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPDC, Maria Mselemu amesema siri ya mafanikio ya ushindi huo, ni kufanya kazi kwa bidii na umahiri.
Akizungumza mara baada ya kupewa tuzo hiyo katika Maonesho ya 49 ya biashara ya Kimataifa, Maria amesema wamekuwa wakifanya vizuri kwenye maeneo tofauti na kupelekea kupata tuzo mara kadhaa.
Kwa mujibu wa Maria, kupitia maonesho hayo, ni mara ya tano 'kunyakua' tuzo hizo.
“Kwetu hii ni tuzo ya tano kwenye maonesho haya lakini sisi kwetu hii ni kawaida kwani tumekuwa tukipata tuzo kwenye maeneo tofauti ikiwamo tuzo ya mazingira,” amesema Maria.
Akizungumzia tuzo hiyo ya mazingira, amesema kufuatia matumizi ya nishati safi ya kupikia wamefanikiwa kuondoa hewa ukaa kwa tani 100,000.
“Kwa kutumia nishati safi ambayo tunaweka kwenye magari lakini pia kupikia pia kufanyakazi kwa umakini ndio kichocheo cha kutufanya kuwa kina," amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED