Jela maisha, miaka 30 kwa kulawiti, kuzini na ndugu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:46 AM Apr 05 2025
Jela maisha, miaka 30 kwa  kulawiti, kuzini na ndugu
Picha: Mtandao
Jela maisha, miaka 30 kwa kulawiti, kuzini na ndugu

Mahakama ya Mkoa wa Lindi, imemhukumu kifungo cha maisha jela, Mkazi wa Wilaya ya Nachingwea, Selemani Hussen Nyuka (32) baada ya kukutwa na hatia ya kumlawiti mtoto wake na kuzini na maharimu (ndugu).

Hukumu hiyo imetolewa Aprili 3, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Delisina Kinath, katika kesi namba 17365/2024.

Katika kosa la kwanza la kulawiti mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha maisha na kosa la pili kifungo cha miaka 30 na kulipa faini ya Sh. milioni 2 kwa mwathirika wa tukio hilo.

Awali, mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani  Juni 25, 2024, ambapo alikana mashtaka yote na kupatiwa dhamana, lakini hata hivyo hakurejea tena mahakamani kwa ajili ya kuendelea na kesi yake, hali iliyopelekea mahakama kutoa hukumu hiyo kwa kukosekana kwake.

Imeandikwa na Salma Mkalibala, MTWARA