Samia aridhia Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma kupumzika

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 04:16 PM Apr 05 2025
Rais Samia Suluhu akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma katika uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama.
PICHA: MTANDAO
Rais Samia Suluhu akiwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma katika uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama.

Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia Jaji Mkuu Prof.Ibrahim Juma kustaafu na kuwataka Majaji kujipanga huku akieleza namna alivyofanya mageuzi makubwa kwa mahakama nchini.

Ameyasema hayo leo jijini Dodoma katika uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama, Tume ya Utumishi wa Mahakama na Nyumba za makazi ya Majaji.

“Najua Jaji Mkuu umebakisha miezi michache kustaafu na mimi sina dhamira ya kugombana na Mahakimu, Majaji wale nina dhamira ya kukuacha ukaumzike kwa hiyo waheshimiwa Majaji jipangeni tu, Jaji anakwenda kupumzika.” amesema Rais Samia