Rais Samia: Imani ya wananchi kwa mahakama imeongezeka

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 04:29 PM Apr 05 2025
 Jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama nchini.
PICHA: IKULU
Jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama nchini.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema imani ya wananchi kwa Mahakama imeendelea kupanda kila mwaka na kwa mwaka 2024 imefikia asilimia 88.

Ameyasema hayo leo jijini Dodoma katika uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama, Tume ya Utumishi wa Mahakama na nyumba za makazi ya Majaji.

Amesema “Tathmini tunayofanyiwa kimataifa imani ya mahakama kwa watu inapanda kila mwaka na hadi mwaka jana imefikia asilimia 88 na naamini maboresho haya yataongeza imani ya watu kuhusu mahakama zao.

 “Lazima tuwajengee imani wananchi kuwa mahakama ndio kimbilio lao la kwanza na la mwisho na la kipekee katika kudai haki.”

Aidha, amehimiza uadilifu kwa watendaji wa mahakama ili kujenga imani ya watanzania kwa mahakama zao na kulinda heshima ya mahakama.