Tundu Lissu: Tukienda kwenye uchaguzi tutaumia bure

By Enock Charles , Nipashe
Published at 06:43 PM Apr 05 2025
Wananchi katika jimbo la Mtama mkoani Lindi wakimsikiliza, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu
PICHA: MTANDAO
Wananchi katika jimbo la Mtama mkoani Lindi wakimsikiliza, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amewataka wananchi wa jimbo la Mtama mkoani Lindi kupigania mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi ili kuwa na ushindani huru na haki.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara mkoani humo leo katika mwendelezo wa ziara za chama hicho kuwaelimisha wananchi kuhusu ‘no reforms no election’ yaani bila mabadiliko hakuna uchaguzi Lissu amesema hawataingia kushiriki uchaguzi wakijua haki haitatendeka.

“Hatuogopi uchaguzi mimi nimegombea tangu mwaka 1995, nilikuwa kijana mdogo nikiwa na miaka 27, nikafanyiwa rafu nikashindwa nikarudi tena, nikarudi tena, nikachaguliwa ubunge mwaka 2010” 

“Nikafanya kazi ya ubunge miaka mitano, nikarudi mwaka 2015 nikachaguliwa mbunge tena kwahiyo mtu anaesema hawa CHADEMA wanaogopa uchaguzi hebu fikiria haya” -Tundu Lissu.