Mgombea urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amepokea zawadi kutoka kwa wananchi wa Mombo, jimbo la Korogwe Vijijini, mara baada ya kumaliza kuzungumza nao katika mkutano wa hadhara.
Wananchi hao walimkabidhi zawadi hizo kama ishara ya upendo na kuonesha mshikamano wao naye, wakati akiendelea na ziara ya kampeni katika mikoa ya Kaskazini.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED