Mgombea Mwenza wa urais kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) ameendelea na ziara yake ya kutafuta udhamini katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Katika maeneo ambayo wagombea wa chama hicho wamepita, Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi ili kuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani na utulivu.
Wagombea wa CHAUMMA walianza safari ya kuomba udhamini katika mikoa miwili ya Zanzibar, na sasa wanaendelea na mikoa minane ya Tanzania Bara, wakitafuta ridhaa ya wananchi ili kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Akizungumzia mchakato huo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Umma wa CHAUMMA, John Mrema, amesema: “Tuache visasi vya siasa, tuache wananchi wachague wenyewe.”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED