Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ampongeza Rais Samia

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 02:55 PM Nov 15 2025
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mpinduzi (CCM) Taifa, Fadhili Maganya
PICHA: PAUL MABEJA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mpinduzi (CCM) Taifa, Fadhili Maganya

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mpinduzi (CCM) Taifa, Fadhili Maganya amepongeza hotuba iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan jana wakati akihutubia na kulifungua rasmi Bunge la 13.

Maganya, ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari akidai kuwa imetoa mwanga mpya kwa Watanzania kutokana na vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi mkuu mwaka huu, zilizosababisha uharibifu wa mali, miundombinu na baadhi ya watu kupoteza maisha. 

Amesema, kitendo cha Rais Samia kubainisha wazi kuwa yupo tayari kuendelea kunyoosha mkono wa maridhiano ni dhahiri kuwa ameumizwa na hali hiyo.Maganya, amesema wao kama Jumuiya ya Wazazi wamepokea kwa mikono miwili kwakua ni njia ambayo itasaidia kuleta umoja na mshikamano na kutibu maumivu ya Watanzania.

“Sisi tunaipokea kwa mtazamo chana kauli ya Rais Samia kwani ametoa kauli ile kama mama na kama mzazi kuhakikisha kuwa analitibu taifa kutokana na mambo ambayo yalitokea wakati wa uchaguzi mwaka huu.
“Tunatoa wito kwa Watanzania wenzetu hasa vijana kuacha kufuata mkumbo na kuhatarisha amani ya nchi yetu lazima tushirikiane pamoja kuendelea kuenzi amani na kuleta mshikamano miongoni mwetu,”amesema Maganya

Aidha, Mwenyekiti huyo amepongeza hatua ya Rais Samia kuwasamehe baadhi ya vijana ambao walihusika katika vurugu hizo na kukamatwa kwa makosa ya uhaini.