Mwinyi arejesha fomu Urais Zanzibar

By Rahma Suleiman , Nipashe
Published at 01:34 PM Sep 06 2025
Mwinyi arejesha fomu Urais Zanzibar
PICHA: RAHMA SULEIMAN
Mwinyi arejesha fomu Urais Zanzibar

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi, leo Septemba 6 amerejesha fomu ya kugombea nafasi ya urais baada ya kukamisha taratibu ikiwemo kupata wadhamini 200 kwa kila mkoa ambapo Zanzibar ina jumla ya mikoa mitano.

Dk Mwinyi amerejesha fomu hiyo majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar Maisara akiwa mgombea wa kwanza kuchukua na kurejesha fomu hiyo kati ya wagombea wote 17 waliojitokeza.

Dk Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhisha fomu hoyo ZEC Dk Mwinyi amesema kuwa idadi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kumdhamini wamepindukia kiwango halisi kilichohitajika na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Akizungumzia kuhusu kauli za baadhi ya wagombea wezake wa vyama vyengine vya siasa waliosema kuwa wameingia katika kinyanganyiro hicho kwa ajili ya kupata umakamo wa kwanza na sio Urais kwasababu hawatoweza kuishinda CCM amesema hilo halina mjadala wowote kuwa yeye ndie anaekubalika kwa wananchi wq Zanzibar.

Aidha amewataka wagombea hao wanaoutaka umakamu wa kwanza kujitahidi kupata kura asilimia 10  kwa sababu wagombea ni wengi na nafasi ni moja.