Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza Jeshi la Polisi usalama barabarani kuendelea kusimamia sheria kwa makini ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika, ikiwemo kufuta kabisa leseni kwa madereva wenye makosa yanayochukua uhai wa watanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye Channel ya Rais Samia, ametoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao katika eneo la Mamba,Kata ya Msangeni wilayani Mwanga.
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya barabarani iliyotokea leo Aprili 3, 2025, katika eneo la Mamba Msangeni, Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, na kusababisha vifo vya watu nane na majeruhi 41,"amesema.
Rais Samia amesema: "Natuma salamu za pole kwa wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali hii. Naendelea kuwasihi watumiaji wote wa barabara kuendelea kuwa waangalifu na kufuata sheria za usalama barabarani."
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED