UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, umewataka vijana wasitumike vibaya kisiasa kuvuruga uchaguzi mkuu 2025.
Wamesema kuna moja ya chama cha upinzani, kimepanga kuvuruga uchaguzi huo, wakisema hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Naibu Katalambula, amebainisha hayo Aprili 8, 2025 mara baada ya Mwenyekiti wa Umoja huo, Abdulaziz Sakala, kumaliza kuzindua Shina la Mama Kata ya Chamaguha,katika ziara yao ya Mama Full Box Oparesheni.
"Wananchi uchaguzi mkuu utakuwapo kwa mujibu wa Katiba na hawa wapinzani wameona hawana hoja kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan, kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo kwa wananchi," ameongeza.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abdulaziz Sakala, amesema uchaguzi huo, CCM watashinda kwa kishindo sababu miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa kwa wananchi.
Ziara hiyo ya UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, imelenga kuzindua mashina ya Mama katika Kata zote 17 za Manispaa ya Shinyanga.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED