MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdallah, amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa Kampeni ya msaada wa kisheria kuwafikia wananchi wa Mkoa wa Tanga hatua ambayo itawezesha kupata Suluhu ya changamoto zao.
Ustaadh Abdallah amewasilisha shukrani hizo kwenye Viwanja vya Tangamano jijini, Tanga na kusema licha ya Kampeni hiyo kufika maeneo mbalimbali nchini wananchi wa Tanga walisubiri kwa hamu kufikiwa na huduma hiyo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED