CHANGAMOTO ya tamaa za kitoto imetajwa kuwa sababu kubwa za mabinti zaidi ya 30, kupata ujauzito katika umri mdogo.
Athari zake na kuacha shule huku wakishindwa kutimiza ndoto zao katika Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.
Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na mabinti wilayani humo wakati wakiongea na vyombo vya habari leo kabla ya kupokea vifaa mbalimbali vya ushonaji na kilimo vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa shirika la Misaada la Uswis-Swiss Contact baada ya kupatiwa mafunzo ya darasani na vitendo.
Zainabu Magwila (30) ni mmoja kati ya wamama wadogo 30 waliokuwa kwenye mafunzo hayo ambaye anaishukuru Swiss Contact ambao walimpatia vifaa vya saluni awali ambavyo vinamsaidia kuendeleza biashara yake na kulisha huku akisomesha Watoto wake watatu bila kuwa na wasiwasi wowote.
Anasema alipata mimba ya kwanza baada ya kuwa na tamaa za kitoto za vitu mbalimbali vidogovidogo akiwa na miaka 17 wakati yupo kidato cha pili na kwamba kabla hajapata fursa ya mafunzo ya kujiamini kutoka Swiss Contact aliishi maisha magumu na familia yake baada ya mwanaume aliyezaa nae kumuacha akiwa na Watoto watatu.
Swaumu Mkoko (24) ambaye amepokea vifaa vya ushonaji anadai alipata mimba akiwa kidato cha tatu kutokana na tamaa za kitoto na kudanganywa na vitu vidogo vidogo vya kula kama vile chipsi na vingine vya kutumia.
Meneja wa Shirika la Swiss Contact Tanzania kupitia mradi wa mwanamke na ujuzi Herman Mshamu amevitaja vifaa vilivyogawiwa kuwa ni pamoja na kinamana wadogo 16 wilayani humo kuwa ni pamoja na vyerahani 10, mashine ya zigzaga 1 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10.
Awali akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Wakili Dunstan Kyobya Afisa Tarafa Wilaya ya Kilombero Fabius Byamungu anawataka kinamama wadogo hao kutojiingiza kwenye vitendo viovu tena kwa sababu serikali na wadau wapo tayari kuwasaidia ili waweze kusonga mbele kimaisha.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED