Hadi Feb 2025 w'biashara 63,222 wasajiliwa

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 06:45 PM Apr 09 2025
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Picha: Mandao
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

SERIKALI imeendelea kutekeleza mkakati wa kuwatambua, kuwasajili na kuwaendeleza wafanyabiashara ndogo.

Hadi Februari 2025, tayari wafanyabiashara 63,222 wamesajiliwa.

Aidha, shilingi bilioni nane zimetolewa na serikali kwa ajili ya mikopo yenye mashartinafuu kwa wafanyabiashara ndogondogo.

“Hadi kufikia Februari, 2025 wafanyabiashara ndogondogo 1,008 wamepata mikopo hiyo,”.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema hayo leo, Aprili 9, 2025, bungeni jijini Dodoma, wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2025/2026.