Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameitangaza rasmi serikali itaunda Tume maalum ya kuchunguza chanzo cha vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu, vurugu ambazo zilisababisha vifo na majeruhi miongoni mwa wananchi.
Rais Samia alisema hayo leo bungeni jijini Dodoma, wakati akifungua rasmi Kikao cha 13 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano.
“Mimi binafsi, waheshimiwa wabunge, nimehudhurishwa sana na tukio lile. Natoa pole kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao. Naomba Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani, na majeruhi tunawaombea wapone mapema. Pia wale waliopoteza mali zao tunawaombea wawe na uvumilivu mkubwa,” alisema Rais.
Akaongeza kuwa, “Serikali imechukua hatua ya kuunda Tume ya kwenda kuchunguza ili tujue kiini cha tatizo na taarifa itakayotolewa na Tume hiyo itatuongoza katika mazungumzo ya kuleta amani na maelewano nchini.”
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED