Salum Mwalimu apewa baraka na wazee wa kimila Karatu

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 06:22 PM Aug 22 2025
Salum Mwalimu apewa baraka na wazee wa kimila Karatu

Mgombea urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amekabidhiwa kifimbo cha kimila na wazee wa kimila wa Karatu, ikiwa ni ishara ya baraka na kumtakia mafanikio katika safari yake ya kugombea nafasi ya juu ya uongozi wa nchi.

Shughuli hiyo ya kimila imefanyika leo mjini Karatu na kuhudhuriwa na wafuasi pamoja na wananchi wa maeneo mbalimbali.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kifimbo hicho, Salum Mwalimu alisisitiza dhamira ya chama chake katika kuleta mabadiliko ya kweli kupitia sanduku la kura na si vinginevyo.

“Hatuwezi kuindoa CCM madarakani kwa kupambana nayo mitandaoni. Hawa ni wa kupambana nao bega kwa bega kwenye sanduku la kura. Kama ni kufa, ni bora tufie vitani na siyo kuwasusia uchaguzi, kwa sababu mkifanya hivyo wao wanafurahi. Hili nalisema, na mwenye kunihukumu anihukumu,” alisema Mwalimu.