Mgombea urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amesema imefika wakati wa kufuta fikra za kizamani na kuingiza fikra mpya za kizazi kipya Ikulu.
Ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wa kampeni uliofanyika Tarakea, jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro, akisisitiza kuwa bila mabadiliko hayo Watanzania wataendelea kubaki katika umasikini.
Mwalimu amesema kuingiza fikra mpya katika uongozi wa taifa kutasaidia kuanzisha mifumo bora ya uzalishaji ajira, pamoja na shughuli mbalimbali zitakazowawezesha wananchi kujiajiri na kuajiriwa ili kujiingizia kipato.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED