Tarimo aahidi kushirikiana na Shayo kuipa ushindi CCM Moshi Mjini

By Mary Mosha , Nipashe
Published at 12:59 PM Aug 26 2025
Tarimo aahidi kushirikiana na Shayo kuipa ushindi CCM Moshi Mjini

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Priscus Tarimo, ameweka bayana dhamira yake ya kushirikiana kwa karibu na mgombea ubunge wa sasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ibrahim Shayo, (Ibra line) ili kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza wakati wa hafla ya uchukuaji fomu ya kugombea ubunge katika Manispaa ya Moshi, Tarimo alisisitiza kuwa hana kinyongo, bali anaendelea kuwa na moyo wa kulitumikia chama na wananchi kwa maslahi mapana ya taifa.

"Naahidi kushirikiana naye bega kwa bega. Ushindi wa CCM ni ushindi wa wananchi wa Moshi. Lazima tuweke pembeni tofauti binafsi na kuweka mbele maslahi ya watu wetu," alisema Tarimo huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.