Wanasayansi watano wa Kitanzania wa utafiti wa magonjwa akiwamo aliyebuni mfumo wa Akili Unde (AI), kupima malaria, wametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD).
Taarifa ya Taasisi ya Afya Ifakara (IHI), iliyotolewa jana jioni imesema mafanikio ya wanasayansi hao yataboresha afya ya umma kupitia utafiti wao wa kisayansi.
Taarifa hiyo imewataja wataalamu waliotunukiwa shahada hiyo kuwa ni Dk. Issa Mshani, Dk. Joel Odero, Dk. Najat Kahamba, Dk. Andrea Kipingu na Dk. Emmanuel Mwanga.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya IHI, wanasayansi wametunukiwa PhD na Chuo Kikuu cha Glasgow cha Uingereza, ambacho ni miongoni mwa vyuo vikuu vinavyoongoza duniani katika nyanja ya utafiti.
“Tunawapongeza kwa dhati watafiti wetu kwa hatua hii kubwa. Mafanikio yao si ya binafsi tu, bali ni ya taasisi na taifa kwa ujumla, kwani yanabeba matumaini ya kuboresha afya na maisha ya mamilioni,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imesema Dk. Mshani ni mwanasayansi ambaye alitumia teknolojia ya akili unde (AI), kuboresha uchunguzi wa ugonjwa wa malaria, kupitia programu ya Deep Diagnostics.
Tayari ubunifu wake umejaribiwa katika vijiji 40 nchini na kusaidia utambuzi wa haraka wa malaria, na kwamba lengo lake ni kutatua changamoto za uchunguzi maeneo yenye upungufu wa vifaa na wataalamu.
Kwa upande wa Dk. Odero, ametoa mbinu madhubuti na endelevu za kudhibiti mbu waenezao malaria.
Dk. Najat, ametoa suluhisho la kisasa la kibaolojia na kijenetiki, kukabiliana na usugu wa viuadudu hususani mbu.
Naye Dk. Mwanga amejikita kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele ukiwamo wa mabusha, kwa kutumia teknolojia mpya kufuatilia mwenendo wa maambukizi.
Utafiti wake umefungua milango ya ushirikiano mpana na nchi nyingine barani Afrika, katika juhudi za kutokomeza magonjwa hayo kwa kutumia uchunguzi wa mapema na zana za kisasa.
Kwa upande wa Dk. Kipingu, ametumia mfumo wa kihisabati kudhibiti mbu katika mazingira mbalimbali, akilenga kusaidia kupanga na kutekeleza mikakati bora ya kuzuia maambukizi kulingana na hali ya kijiografia na ikolojia ya maeneo husika.
Kuhusu Chuo Kikuu cha Glasgow, taarifa hiyo inasema kilianzishwa mwaka 1451 na kinajulikana kwa mchango wake katika utafiti wa kisasa wa tiba, afya ya kimataifa na sera za umma.
Na Restuta James
WANASAYANSI watano wa Kitanzania wa utafiti wa magonjwa akiwamo aliyebuni mfumo wa Akili Unde (AI), kupima malaria, wametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD).

© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED