Mwalimu aliyetumia wimbo wa Pawa kufundishia apongezwa

By Grace Mwakalinga , Nipashe
Published at 01:17 PM Aug 19 2025
Wizara yampongeza mwalimu kutumia wimbo wa Pawa kufundishiatu.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imempongeza Mwalimu Jao Kalesi wa Shule ya Msingi Kazita, wilayani Muheza mkoani Tanga, kwa ubunifu wa kutumia muziki kufundishia wanafunzi darasani.

Mwalimu huyo ametumia wimbo maarufu wa msanii wa Bongo Fleva, Mbosso Khan, uitwao Pawa, kuingiza maudhui ya kielimu yenye lengo la kuwahamasisha na kuwajengea wanafunzi ari ya kujifunza.

Wizara imesisitiza kuwa sanaa kwa sasa ni nyenzo muhimu katika sekta ya elimu, ikiwemo muziki unaoweza kutumika kama daraja la kufundishia na kuhamasisha wanafunzi kufahamu masomo kwa urahisi na kwa njia ya kuvutia.