WAKATI zimebaki siku chache kwa Watanzania kushiriki katika tukio muhimu la kupiga kura hapo Oktoba 29, ni lazima umakini uwapo kuepuka kujiingiza katika habari za uongo na uzushi. Kutokana na mabadiliko ya teknolojia, kila mtu hivi sasa anaweza kutuma habari au picha yoyote kwenye mitandao ya kijamii ili mradi awe anamiliki kifaa cha mawasiliano.
Teknolojia imeleta mageuzi makubwa, lakini kuna faida na hasara zake ambazo kama wananchi wasipokuwa makini wanaweza kujiingiza katika mtego wa kushtakiwa na hatimaye kufungwa au kulipishwa faini kubwa.
Mafanikio yaliyopatikana ni watu kupata fursa nyingi za kujifunza kupitia mitandao hasa inapotumika vizuri na wengine kutengeneza ajira ambazo zinawapatia vipato.
Vilevile, matumizi hayo yalisaidia kipindi ambacho dunia ilikumbwa na janga la Uviko na kusababisha wafanyakazi kuathirika na baadhi yao kupunguzwa kazi huku wengine wakilazimika kufanya kazi zao wakiwa nyumbani.
Teknolojia hiyo pia imesaidia masomo na mikutano kufanyika mitandaoni badala ya kukutana uso kwa uso na kuokoa gharama za watu kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine.
Hayo ndiyo matumizi mazuri ya teknolojia ambayo yanaleta tija kwa watu na nchi pia. Hata hivyo, baadhi ya watu wanaitumia vibaya teknolojia hiyo kwa kurusha vitu vinavyozua taharuki na kuchafua watu wengine hasa kipindi hiki cha uchaguzi.
Kuna mambo mengi yanayotokea katika kipindi hiki huku wahalifu wakitafuta mbinu mbalimbali za kuhakikisha wanakwenda sambamba na mabadiliko hayo.
Dunia kwenda na mabadiliko ya teknolojia ni kurahisisha kazi na kupunguza muda unaotumika kwa binadamu kuifanya kazi hiyo.
Pia, wapo wanaotumia picha za matukio ya zamani na kuzitengeneza ili mradi kuwachafua watu na kuwaharibia wasifu wao. Teknolojia hii isitumike kuharibu badala yake itumike kuji
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED