Rais Samia ampongeza Alphonce Simbu ushindi Boston Marathon

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:56 AM Apr 22 2025
Rais Samia ampongeza Alphonce Simbu ushindi Boston Marathon
Picha: Mtandao
Rais Samia ampongeza Alphonce Simbu ushindi Boston Marathon

Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa pongezi za dhati kwa mwanariadha Alphonce Simbu kwa kushika nafasi ya pili katika Mashindano ya Kimataifa ya Mbio za Boston (Boston Marathon) yaliyofanyika hivi karibuni nchini Marekani.

Kupitia salamu zake, Rais Samia amesema:

"Pongezi za dhati kwa Alphonce Simbu kwa kushika nafasi ya pili katika Mashindano ya Kimataifa ya Mbio ya Boston (Boston Marathon). Umefanya kazi nzuri."


Ameongeza kuwa ushindi huo si wa bahati nasibu, bali ni matokeo ya juhudi kubwa, maandalizi ya hali ya juu, na nidhamu ya mfano ambayo Simbu ameionesha tangu akiwa jeshini, katika mazoezi na hadi kwenye mashindano yenyewe.

"Ushindi wako ni matokeo ya kujituma kwa bidii, maandalizi mazuri, nidhamu yako kuanzia jeshini, kwenye mazoezi hadi kwenye mashindano, ukilibeba kwa heshima ya hali ya juu jina la nchi yetu," alisema Rais Samia.


Rais amepongeza ari na uzalendo wa Simbu na kumtaka aendelee kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa, akisisitiza kuwa mafanikio yake ni chachu kwa wanamichezo wengine nchini.


"Endelea kuipeperusha vyema bendera ya Taifa letu," amehitimisha Rais Samia.