Chalamila atangaza zawadi nono kwa Taifa Stars

By Imani Nathaniel , Nipashe
Published at 01:22 PM Aug 22 2025
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.
Picha: Imani Nathaniel
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametangaza kutoa zawadi ya shilingi milioni 20 pamoja na viwanja viwili kwa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) mara baada ya kufuzu hatua ya robo fainali, huku akiahidi motisha zaidi kulingana na matokeo ya mchezo wa leo dhidi ya Morocco.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Chalamila amesema kila bao litakalofungwa katika mchezo huo litazawadiwa shilingi milioni 5, ambapo mfungaji atapokea shilingi milioni 1 na mtoa pasi ya bao (assist) atapewa shilingi 500,000.

Aidha, amebainisha kuwa kipa atakayefanikisha kuzuia bao bila kuruhusu nyavu zake kuguswa atajinyakulia zawadi ya gari aina ya Toyota Crown.

“Zawadi hizi ni ishara ya heshima kubwa kwa Taifa Stars kwa kuendelea kutuwakilisha vyema. Nawashukuru kwa kushinda michezo mitatu mfululizo. Nawasihi Watanzania wote tujitokeze kwa wingi kushangilia timu yetu,” amesema Chalamila.
1