Mbeya yawatuliza mashabiki wake

By Grace Mwakalinga , Nipashe
Published at 05:27 PM Aug 14 2025
Ofisa Habari wa Klabu ya Mbeya City, Gwamaka Mwankota.
Picha: Grace Mwakalinga
Ofisa Habari wa Klabu ya Mbeya City, Gwamaka Mwankota.

KLABU ya Mbeya City, imetoa ufafanuzi kuhusu picha za jezi za mazoezi zinazoonekana kwenye mitandao ya kijamii, ikiwamo ukurasa rasmi wa klabu, ikivaliwa na wachezaji wake.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Gwamaka Mwankota, ameeleza kuwa jezi hizo ni maalum, kwa ajili ya mazoezi pekee na siyo jezi rasmi za mashindano.

Mwankota amebainisha kuwa jezi rasmi za Mbeya City kwa msimu mpya wa Ligi Kuu 2025/2026, zitazinduliwa rasmi hivi karibuni.

“Tunawaomba wapenzi, mashabiki na wadau wa mpira wa miguu wakae tayari kwa ujio wa jezi zetu mpya, zenye ubora wa hali ya juu, zitakazopatikana ndani na nje ya nchi,” amesema Mwankota.

Klabu inasisitiza kuwa itatoa taarifa zaidi kuhusu namna ya kununua jezi hizo ili kuhakikisha kila shabiki anaweza kuzipata kwa urahisi.