TFF kuja na mshirika wa michezo ya kubashiri msimu wa 2025/26

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:54 PM May 12 2025
TFF kuja na mshirika wa michezo ya kubashiri msimu wa 2025/26
Picha: Mtandao
TFF kuja na mshirika wa michezo ya kubashiri msimu wa 2025/26

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa kuanzia msimu ujao wa 2025/2026, litakuwa na mshirika rasmi wa michezo ya kubashiri kwa ajili ya mashindano yote yanayosimamiwa na shirikisho hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, mshirika huyo atapewa haki ya kipekee ya kutoa huduma za kubashiri kwa kipindi chote cha makubaliano. Hii ina maana kuwa taasisi au kampuni yoyote itakayohitaji kuweka “odds” (alama za ubashiri) kwa mechi zitakazokuwa chini ya TFF, italazimika kuwasiliana moja kwa moja na mshirika huyo.

TFF imesisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza usimamizi bora wa taarifa za mechi, kuongeza mapato ya mashindano, na kuhakikisha mashirikiano yenye manufaa kwa pande zote — wachezaji, vilabu, wadhamini, na mashabiki.

Majina ya kampuni au taasisi zitakazoshiriki katika mchakato wa kupata nafasi hiyo ya ushirika yanatarajiwa kutangazwa hivi karibuni baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria na kiutawala.

Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)@taifastars_ @caf_online @ligikuu @bonwambura70.jpg 206.8 KB