DHANA na tendo la mauaji katika jamii, huwa linabeba ukakasi mkubwa, hofu na chuki. Pia, tukigeuza mbele ya imani zetu, bado nazo zinakemewa sana.
Mtazamo tunapaswa kusimamia wote ni kwamba jamii inatakiwa kufunguka, huku ikishirikiana na mamlaka husika ambayo ni serikali, katika kukomesha matukio ya mauaji kila kona.
Hapo tunapaswa kujua kila inapotokea mauaji hayo, ina maana kwamba yanawapa shida wengine wengi.
Tujiulize hili linaanzia wapi! Tafakari ya marufuku huanzia penye ulimbukeni au makusudi ya kujichukulia sheria mkononi kumwadhibu mwingine. Hilo huangukia ama madhara au hata kifo.
Ni bahati mbaya, ndiyo matukio tunayasikia hapa na pale madhara, hata vifo.
Wacha nikumegee kidogo, kuna chuki ambazo watu hujiwekea vichwani mwao, pasipo kujali kuwa wanaweza kuleta madhara makubwa hatima yake kuwa mbaya.
Hiyo haijalishi hata nyuma ya pazia. kulikoni hiki na kile kundi la jamii linadhuriana, iwe wivu wa mapenzi, kudhulumiana, tamaa za mali na mengine mengi kama kusambaa hisia za ugomvi na visasi.
Kwa mapana, niseme hatua hiyo unapoenda kumdhuru mwingine, ujue nawe katika nafasi yako unakuwa hatarini maana madhara yanaweza kukurudia, hata ikiwezekana suala la kifo.
Uso wako kwa Muumba, nako kuna hatari yake, imani zetu wote, zinakemea mabaya hayo.
Waungwana nifunguke, hakuna namna au mantiki ya kufanyika mauaji, watu wengine wanabaki na upweke, pasipokuwa na sababu za msingi je umewahi kufikili pindi mauaji yanapotokea wanaobaki wanakuwa wapo kwenye wakati gani.
Wapo watu wanaosimamia upweke mpaka leo, hasa pale wanapokumbuka namna wapendwa wao walivyopoteza maisha na imani, ikizama kwa kina, jamani matukio hayo yanaumiza.
Ndio maana hata kiongozi wetu nchini, kwa mana ya mkuu wa nchi wakati fulani, amekemea vikali matukio hayo yasiyostahili kwenye jamii zinazotuzunguka.
Siyo siku nyingi tukasikia ya kushitua, matukio ya kutisha na kuumzia nafsi za watu, kukirekodi idadi ya mauaji katika mikoa kama ya Mtwara, Mbeya, Mwanza, Moshi na Dodoma.
Nakumbuka mwaka jana, wakati Jeshi la Polisi nchini linaadhimisha miaka 60 ya kuwapo kwake, mkuu huyo wa nchi akadai kuwapo uchunguzi dhidi ya mauaji hayo yanayojenga picha isiyopendeza kijamii.
Sote wanajamii, raia tukiunda kundi kubwa tunatakiwa kuwa kioo kwa jamii, tukishirikiana na serikali katika kupambana na kufichua uhalifu huo.
Najua baadhi yetu tunaishi na hao wanaofanya madhara, hata wanainyima usingizi serikali. Hivyo, hata lile jukumu la kuonyesha wanaofanya hayo ni kina nani, ni letu sote.
Tunapaswa kukumbuka hata maandiko yetu kiimani, yanahimzia utulivu. Tunatakiwa kujifunza kusamehe na kuwa walimu kwa wengine ili kupata kizazi kilicho bora tusiwe watu wa vinyongo na visasi, kumwaga damu ya mtu mwingine, bila ya sababu au kuna hatua bado haipendezi.
Siku hizi zipo kuwapo jambo kwenye mikono ya sheria epukeni tamaa za mali, wivu wa mapenzi. Wanajamii simameni kuwa kioo ya kufichua uovu.
Iwe utashi wetu kuanzia ngazi ya mahali tuliko, kisha ikapanda ngazi katika serikali za mitaa, hadi kufika serikali kuu na mfumo mpana nguzo ya usalama wa kitaifa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED