Hongera tunaiona siasa yetu, tujifunze Oktoba 29 tuboreshe

By Tuntule Swebe , Nipashe
Published at 12:59 PM Sep 04 2025
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozindua uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, katika uwanja wa Kawawa, mkoani Kigoma
Picha: OWM
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozindua uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, katika uwanja wa Kawawa, mkoani Kigoma

SASA ni ama zama au msimu wa uchaguzi mkuu nchini. Kila mmoja anaweza kutumia sentensi ya namna yake, lakini maana inabaki palepale.

Siku mahsusi ni ile inayotajwa kuwa Oktoba 29, ikiwa chini ya miezi miwili kuanzia sasa. Namba moja, mtu akiniuliza cha kujivunia, sihitaji hata kukuna kichwa, ni ‘ndani ya amani,’

Niseme jambo la kujivunia, wazalendo nchini wenye taifa zuri na uhuru wa siasa, tunaona yanayoendelea kwenye demokrasia yetu.

Wigo huo mpana umewabeba wanasiasa ‘kindakindaki’ baadhi kuwapa uhuru wa kujiunga na chama pasipo kupingwa na yeyote yule.

Sio tu kujiunga, bali hata kama vyama vyote vikidumu kusimama katika mstari, vinaweza kufuata haki na sheria, hali kadhalika sera rafiki zinazoendana na matakwa ya nchi.

Bado upana huo umewabeba wadau hao kwa kuwapa uhuru wa kujinadi. Hata hivyo inapendeza sana, kwa sababu hawajali jinsia, dini, wala kabila.

Kihistoria, zama za uongozi kitaifa nchini zimejumuisha viongozi waliopita madarakani katika mitazamo ya namna tofauti, lakini inapokuja wanawafanyia nini Watanzania, wanaangukia sera na mtazamo wa kusonga mbele kwenye maendeleo ya nchi.

Rais wa Awamu ya Kwanza, Julius Kambarage Nyerere kiimani alikuwa tofauti na wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi. Lakini ukiwajumuisha kwa yaliyobaki, wamekuwa wakiimba wimbo mmoja, kitikadi, amani hadi staili ya kusaka maendeleo nchini.

Hiyo ndiyo inasonga hadi kwa waliowarithi kufika ngazi za juu. Ni vema kutambua namna ya kuwapo jambo kwamba serikali imekomesha udini na ukabila na zao hali lipo lenye umri wa miaka 61, Tanganyika na Zanzibar kuungana zikaunda taifa Tanzania, ikiwa ni Jamhuri ya Muungano.

Watu wamepewa usawa wa kujiamini na kuwa uhuru kwenye kugombea nyazifa mbalimbali ikiwamo ngazi za serikali za mtaa mpaka serikali kuu.

Kinachofanyika sasa ni kwamba, moja ni nafasi hasa kwa walio wageni kujifunza namna demokrasia inavyotumika katika njia nzuri hata kuwa kigezo wenye nia kusajili vyama vya siasa au kujitosa kwa wadau siasa.

Ndani yake waibuke kufuata sheria, pia katiba ya nchi, pasipo kusahau historia na vigezo nchi tulikopita.

Kigezo kikuu cha kufanikiwa mara zote, tusifanye kitu kwa kukurupuka, bila ya kuweka mitazamo hasi. Inafaa kuhakikisha kuwa unachokifanya una uhakika nacho.

Mtanzania aliyegubikwa na uzalendo kwenye taifa lake, afanyapo siasa ni lazima kuegemea sheria na taratibu, ikiwamo kuwa na chama cha siasa alichojiunga nacho, ili kuweza kupambania maslahi ya nchi. Bila shaka tunayo nafasi!

Tuachane na ngonjera zisizojenga hata kujiwekea, tufike mbali kwa kuchagua mgombea na chama unachokipenda na kuwapo sababu na hoja zinazozugumzika.

Pia, hauwezi kujua kwamba, kura yako moja ndio ushindi kwa yule unayempenda na hiyo ndio siri ya ushindi. 

Tunatakiwa kusimamia nafasi zetu kizalendo, bila kujali kuwa mbona fulani yupo mahali fulani au kitu hiki kiko vile.

Kwa mapana, wale wanaotaka kuanzisha vyama vya siasa nafasi zipo, ili mradi wanatimiza vigezo, masharti na kanuni. 

Safari kuelekea uchaguzi mkuu ujao inatakiwa kumaliza kasoro, kwa sasa au huko twendako.

Vyama navyo vinatakiwa kutoa uhuru kwa kila Mtanzania mfuasi wake - mwanachama, katika usawa wote wa kidini, jinsia,kidini, kiitikadi ajitose kuwania nafasi ya uongozi anayonuia.

Jamii tunatakiwa kuamka na kuwa wazalendo kwa kujisajiri kwenye vyama vya siasa na kwa wakeleketwa kubuni vyama vyao kwa kufuata sheria Niseme tu, hongera tulikofika, tunaiona siasa yetu, tujifunze Oktoba 29, tuboreshe zaidi.