NENO kuwajibika katika jamii, ni kutokuwa katika hali ya kujilegeza kushughulikia jambo, au kutofumbia macho jambo. Mtu anatakiwa kuhamia ile dhana kwamba awajibike ama kwa mazuri au kudhibiti yaliyo mabaya.
Hoja yangu kinachonifanya nami nichukue hatua kwa mabaya ninayoyaona, ni katika kukuhabarisha juu ya tabia inayoonekana kuganda kama luba, kwenye baadhi ya mitaa ya mjini Dares Salaam, kukiwamo fukuto hilo.
Kuna mitaa na nyendo zake inakera sana hata kushuhudia. Niende moja kwa moja, katikati ya mji huu niliko, kuna ushuhuda wa mfano, kama sokoni Kariakoo na kwingineko penye masoko kama Ilala boma na Mwenge. Huwa ninawaona wanaopaswa kwenda shule, wanashinda barabarani wakiomba pasipo kujua hatma yao ni ipi.
Jambo la kustaajabisha familia, wapo wanaotumia watoto kuweza kupata faida. Je tunajua namna kwenye eneo langu la mfano Mwenge, ikijaribu kudodosa na kugundua watoto hao wanatumika kama namna ukombozi wa kusaidia familia zao. Bila shaka tunaanza kuharibu kizazi kwa mikono yetu wenyewe, watu wanatumia kuomba kama fimbo ya kukwamua kiuchumi, pasipo kujali kuwa wanawaumiza wengine, wao na taifa zima.
Tunatakiwa kulitazama hilo kwa jicho la tatu. Hawa jamaa wanawaweka watoto hatarini, kwani kuna hatari ya kugongwa na magari, wakapata majeraha baada ya kusukumwa na mtu, hata kupoteza haki zao za msingi.
Pindi mtoto anapokuwa barabarani, nawaomba enyi wazazi wenzangu tujue wanapoteza haki zao za kupata elimu. Inasikitisha sasa, kwa manufaa ya mtu mwingine ni kwa sababu anatumika kama chombo cha kuweka kipato kwenye familia.
Wazazi na walezi wengine, wanaonekana wakishirikiana watoto hao katika kusongesha gurudumu la maendeleo yao yasiyo na dira ya kusongesha taifa na jamii mbali, wala kujali mazingira hatarishi kwa mtoto Ni hatua tunapoteza watalamu, maana daktari, injinia, mwanajeshi, hata mwanasheria, utaaluma wake unaanzia huko darasa la kwanza.
Watoto hao hawasomi, wanabaki wakizagaa barabarani kwa maslahi ya wakubwa katika familia zao. Inakuwa tabia yao ya kudumu maishani. Kwa mapana, natamka jambo hili ni kichocheo cha nchi kuwa maskini.
Ni sababu ya kuongezeka watu wasiojua kusoma wala kuandika chochote au tafakari ya akili iliyokuwa shule. Hadi sasa Taifa lipo hatarini kuwapoteza watu hao muhimu kwenye nyadhifa zao kitaalamu.
Watoto hao kama wakisoma na kupata usumbufu, kama Taifa lingezidi kuwa juu kwa kuwatumia watu hao. Kurejea uhalisia, kwa sasa taifa liwageukie watoto hao kwa nguvu za kisheria ikiwa na mambo kadhaa.
Kuwaona kwa jicho la vita linafika mbali kukabili matumizi ya dawa za kulevya, kuuza miili yao kwa maana ya ‘makaka poa’ na ‘madada poa’, kando yao kukiwapo magenge ya ualifu. Yote ni kwa sababu wanaviona kutoka kwa watu wengine nao wanaiga, bila ya kufahamu dunia inachohitaji.
Sasa hayo, mwisho wake unaweza kuwa mbaya kutokana na kupoteza kizazi sahihi, kwani wanapotoshwa ilhali hawajitambui, wakifunga macho tayari wamezama kusiko wanaathirika machafu hayo la uvutaji ‘unga’ na kadhalika.
Wazazi na walezi, mjiulize mmewahi kufikiri juu ya adha wanayoipata wadogo hao? Upande wa pili ingependeza watu hawa wanaokaa na familia zao barabarani wakiomba wakachunguzwe na wanasakiolojia wana shida au ni makusudi ya kurahisisha maisha.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED