NDANI ya jamii kumekuwapo na tabia inayokaa, kila kukicha, zikiwa tofauti kwa kuwapo watu wanaotumia mitandao vibaya, wakitoa lugha au kauli chafu kupitia mitandao, dhidi ya watu wengine
Muhimu kukabili hilo ndani ya jamii, inatakiwa ikumbukwe kuwa mitandao inawafikia watu wengi na kunatakiwa kuwapo mipaka ya kuikabili, kwani inaharibu vizazi kupitia mitandao hiyo.
Wanaoitumia kuonesha picha zisizo na maadili, kukamilisha ama malumbano yapo ya tabia ya kuwekwa picha zisizofaa na malumbano yasiyo na jema.
Hivyo basi, kuikabili tunatakiwa kusimama imara kunusuru watoto tulio nao, kwani matukio na vitu vya kuharibu maadili yetu ni mepesi sana kunasa kwa watoto hao. Bila shaka, hali ya watu kukinzana kunatakiwa kutafutiwe mahali na mbadala rasmi ya faragha na nje ya mitandao, kwani kunazusha sintofahamu inayotumbukia kwa watoto hadi watu wazima.
Jamii inatakiwa kuepuka lugha zote chafu zinazoendelea ndani ya mitandao. Nakumbuka huko jijini Dodoma, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima, anawataka Watanzania kuungana katika kudhibiti vitendo viovu.
Akayataja mazingira na mifano husika kama vile kutumia picha mnato au mjongeo zinazoonesha faragha za mwili wa watu, hata kuchangia mmomonyoko wa maadili kijamii. Waziri Gwajima akayaeleza kama usahidi rasmi wa ukiukwaji maadili na sheria nchini, akinena: “Video na picha za watu wanatikisa na kuonesha viungo na mambo.... hadharani.
Ili tuwaoneshe vifungu vyao vya sheria vikoje,” amesisitiza kiongozi huyo. Hata hivyo, anatahadharisha kuwapo wengine aliyosikia wameanza kufuta ‘aibu zao’ ndani ya mtandao kwa kasi kubwa. “Tupate kianzio, maana maneno tumesema na kurudia rudia wamejifanya hawasikii lolote wala chochote na sheria hawajataka kuzisoma,” anahimiza Waziri Gwajima, akitamtaka kuwa, wanaohusika na vitendo hivyo wanafanya kinyume cha sheria, hivyo anashangaa inakuwaje hawakumbuki hata kuwauliza wanasheria lililo jema na lipi baya.
“Haiwezekani tukawa tunasema tu na wao wanafanya tu. Imetosha! Vielelezo, kuna wengine wameshaniletea kadhaa,” anasisitiza. Ni suala linaloshughulikiwa na sheria kadhaa za nchini, zinazodhibiti maudhui ya mtandaoni na kudumisha maadili ya jamii.
Hapo kwa uchache, kuna mfano wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015, inakataza kusambaza maudhui ya aibu, yanayokiuka maadili au kuhamasisha tabia zisizo za kimaadili kupitia mitandao.
Ni sheria inayozuia mambo kama usambazaji picha za utupu au maudhui yasiyofaa mtandaoni na mtu anayekiuka sheria hiyo, anaweza kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria zilizopo. Hapo kuna kama Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010.
Kupitia Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni za Mwaka 2018 (Online Content Regulations), inatoa mwongozo unaodhibiti maudhui yasiyofaa, ikiwamo picha na video kwenye mitandao ya kijamii. Inazuia uoneshaji na usambazaji maudhui yoyote yanayokiuka maadili na mila za Kitanzania mtandaoni.
Ni sheria zinazotoa mamlaka kwa serikali kudhibiti aina ya maudhui yanayoruhusiwa kusambazwa mtandaoni, hata kuhakikisha yanazingatia maadili na usalama wa jamii. Kuna sheria inayonyoosha vidole dhidi ya kutukana au kugombana na wengine kupitia mitandao.
Mdhamini mkuu husika katika yote hayo, ni katika yanayohusu matumizi mabaya ya mitandao Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Katika mtazamo wa jumla, kimaadili wote tusimame kukemea matumizi mabaya ya mitandao, kwa mambo mbalimbali Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA imeonya kuwa itawachukulia hatua kali baadhi ya watu wanaotumia vibaya huduma za mawasiliano ya simu na mtandao wa intaneti, hasa wale wanaodhalilisha pamoja na kuhatarisha amani
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED