Siku kama ya leo, ule mkasa Septemba 11 ulikuwa hivi...

By Beatrice Moses , Nipashe
Published at 12:13 PM Sep 11 2025
Mwonekano wa jengo la World Trade Center baada ya shambulio mwaka 2021 huko Marekani
Picha: BBC
Mwonekano wa jengo la World Trade Center baada ya shambulio mwaka 2021 huko Marekani

MIAKA 24 inatimu leo, tangu kutokea kwa shambulio la tarehe 11 Septemba 2001, likiwa limebeba mashambulio manne yaliyofanywa kwa pamoja na kinachotajwa kikosi cha kigaidi cha al-Qaida, ndani ya Marekani.

Siyo siri, tukivuta hisia nyuma na yale yaliyotokea, ni maafa makubwa yaliyotikisa dunia nzima.

Kwa mujibu wa taarifa kuhusu tukio hilo, watekelezaji kikosi cha Al-Qaida, baada ya kuziteka nyara ndege nne za Marekani, wakazitumia kama silaha za kugonga majengo jijini New York na Washington DC, wahusika wakijitoa muhanga.

 Umati mkubwa wa watu waliokufa, wastani wa makadirio inafananishwa kukaribia mfano wa kijiji kimoja nchini. Ndege zilitumika kufanya ugaidi ikiacha mabaki ya jengo maarufu la WTC.

Nikisimulia mkasa ulivyokuwa! Ndege ya American Airlines Flight 11, ilitumiwa kugonga mnara Kaskazini mwa Jengo la Biashara la Kimataifa (World Trade Center) jijini New York, asubuhi kama ya leo saa mbili na dakika 46.

Ndege ya pili, United Airlines Flight 175, baada ya robo saa, ikatumiwa kugonga mnara wa jengo la Biashara la Kimataifa (World Trade Center) Kusini, saa tatu na dakika mbili asubuhi hiyo hiyo.

Watu wengi waliona tukio la pili, kwa sababu kilichojiri awali kilikwishasambaa katika mji, kamera za televisheni zilielekezwa katika eneo la tukio.

Taharuki ikiendelea, ndege ya American Airlines Flight 77, ikatumiwa kugonga jengo la Pentagon jijini Arlington, Virginia (karibu na Washington DC) saa tatu na dakika 37:46 asubuhi hiyo. Ni bada ya nusu saa na ushee kupita shambulio la pili (baada ya dakika 34), baada kugongwa jengo la World Trade Center.

Kisha tena ndege ya United Airlines Flight 93, majira ya saa nne na dakika tatu, ikiwa ni nusu saa imepita, baada  ya sakata la tatu, lenyewe ‘almanusura’  halikufanikiwa kugonga kokote, wana usalama wakaiwahi kuiangusha chini, saa nne na dakika tatu. 

Inaaminika magaidi hao walitaka kuigonga ndege hiyo katika jengo la mji mkuu wa Marekani.

Abiria walijaribu kuikomboa ndege kutoka kwa magaidi, lakini hawakufanikiwa, matokeo yake wakaishia kuanguka karibu na mji wa Shanksville, Pennsylvania.

Jumla ya abiria 246 na magaidi 19 waliokuwa katika ndege zote nne walikufa.

Pia, ikaibainika katika ndege ya shirika American Airlines 11, ilikuwa na abiria 87 na magaidi watano; United Airlines 175 ilibeba abiria 60 na magaidi watano.

Ndege ya American Airlines 77 ilikuwa na abiria 59 na magaidi watano; vilevile United Airlines 93 ilibeba abiria 40 na magaidi wanne.

Minara yote miwili ya jengo la World Trade Center ilungua baada ya shambulio. Mnara wa Kusini (WTC 2) uliungua kwa dakika 56, kabla ya kuanguka na kuteketea yote.

Jengo la Kaskazini (WTC 1), liliungua kwa saa moja na dakika 42, pia likaanguka. Sehemu na mmomonyoko wa jengo hilo, lilisababisha majengo mengine yaliyoyazunguka nayo kushika moto na kuteketea.

Jengo la tatu la 7 World Trade Center (7 WTC), nalo likaanguka saa 11 na dakika 20 jioni. Baadhi ya majengo mengine jirani, nayo yaliharibiwa na kuteketea.

Takriban watu 2,602 walipoteza maisha katika Jengo la World Trade Center.

Ndege iliyogonga Pentagon iligonga chini mwa upande wa Magharibi mwa jengo hilo. Kisha ikagonga mpaka katika nguzo tano zinazoshikilia jengo hilo la Pentagon, hata kusababisha watu 125 kufariki.

Inaelezwa jumla ya watu 2,973 walikufa katika shambulio hilo, kati yao wamo askari polisi wa jijini New York 23, pia polisi wa bandarini 37, walikuwa wakijaribu kuokoa maisha ya baadhi ya wahanga wa janga hito.

Shambulio hilo linatajwa kuwa kubwa la kwanza kwa watu wasio Wamerekani kufanikiwa kushambulia nchini humo, tangu mnamo mwaka wa 1941, pale Wajapani waliposhambulia Kituo cha Jeshi la Maji katika Bandari ya Pearl, Hawaii. 

Baada ya shambulio, Wamarekani wakawa wanawalaumu Al-Qaeda kwa kitendo walicho kifanya. Tangu hapo wakaianza vita dhidi ya Ugaidi. Kiongozi wa al-Qaeda, Osama bin Laden,