HaloPesa yazindua kampeni mpya “Tamba na Bonasi”

By Zuwena Shame , Nipashe
Published at 07:21 PM Oct 03 2025
HaloPesa yazindua kampeni mpya “Tamba na Bonasi”
Picha:Mpigapicha Wetu
HaloPesa yazindua kampeni mpya “Tamba na Bonasi”

Huduma ya kifedha ya Halotel, HaloPesa, imezindua kampeni mpya iitwayo “Tamba na Bonasi”, ambayo inamtambulisha balozi wa kidijitali anayejulikana kama Mr. Bonus atakayekuwa nembo ya promosheni hiyo.

Kupitia kampeni hii, wateja watajipatia bonasi za kuvutia kwa kufanya miamala ya kila siku kupitia HaloPesa, ikiwemo kutuma na kutoa pesa, kulipia bili, kununua bidhaa, pamoja na kununua umeme (LUKU). Aidha, wateja watashiriki katika droo za kila siku, kila wiki na kila mwezi, ambapo washindi watajinyakulia zawadi ya hadi Shilingi Milioni 2 taslimu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Idara ya Biashara wa HaloPesa, Happy Mzena, alisema kampeni hiyo inaonesha dhamira ya kampuni ya kuendelea kuwapatia thamani kubwa zaidi wateja wake.

“Mr. Bonus siyo tu alama ya kampeni hii, bali pia ni jukwaa la kidijitali la zawadi linaloleta msisimko katika kila muamala. Lengo letu ni kuhakikisha kila huduma ya HaloPesa inampa mteja nafasi ya kushinda,” alisema.

Kwa upande wake, Afisa Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza, alisema kampeni hiyo imelenga kufanya huduma za kifedha za kidijitali ziwe na mvuto na kushirikisha zaidi wateja.

“Tamba na Bonasi ni uzoefu wa kipekee wa kidijitali ulioundwa mahsusi kwa wateja wa HaloPesa. Mr. Bonus analeta burudani na zawadi, kuhakikisha kila muamala unakuwa fursa ya kushinda,” alifafanua.

Aidha, Lwiza alibainisha kuwa HaloPesa inaendelea kuongoza kwa kutoa huduma nafuu, akitaja kuwa miamala kutoka HaloPesa kwenda HaloPesa kupitia App ya HaloPesa ni bure, na vivyo hivyo ununuzi wa umeme.

Pia alisisitiza juu ya usalama wa wateja wakati wa kampeni, akiwakumbusha kuwa taarifa rasmi za ushindi zitatumwa kwa jina la HaloPesa pekee, na simu za kuthibitisha ushindi zitapigwa kupitia namba ya huduma kwa wateja 100.

HaloPesa imesema kampeni hii inaonesha kujitolea kwake kutoa huduma zenye urahisi, usalama, pamoja na zawadi na burudani kwa wateja wake nchini kote. Kupitia mtandao mpana wa mawakala na maduka ya Halotel, kampuni imewahakikishia Watanzania kuwa huduma zake zitaendelea kuwa nafuu na rahisi kupatikana.