JENGO la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) liliko Kariako linatekea kwa moto.
Akizungumzia ajali hiyo leo January 30, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema haijulikana moto huo ulianza kuwaka muda gani japo juhudi za uokozi zinaendelea.
Amesema tayari Jeshi la Uokoji, magari ya zimamoto yameshafika katika eneo hilo na shughuli ya kuuzima moto huo inaendelea.
“Bado hatujabaini nini chanzo cha moto huu, na kwa sasa siwezi kusema chochote mpaka pale tutakapo fanikiwa kuudhibiti kwa sababu vyombo vyote vya dola viko hapa” amesema Kayombo
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED