ISRAEL imekubali ‘masharti ya lazima’ ili kukamilisha usitishaji vita wa siku 60 huko Gaza, Rais wa Marekani Donald Trump amesema.
Wakati wa makubaliano yaliyopendekezwa, "tutafanya kazi na pande zote kumaliza Vita", Trump amesema katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, bila kuelezea masharti ni nini.
"Waqatar na Wamisri, ambao wamefanya kazi kwa bidii sana kusaidia kuleta Amani, watatoa pendekezo hili la mwisho. Natumai... kwamba Hamas itayakubali Makubaliano haya, kwasababu hayatakuwa mazuri – MAMBO YANAWEZA TU KUWA MABAYA ZAIDI," Trump aliandika.
Israel ilianzisha kampeni ya kijeshi huko Gaza baada ya shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israel, huku takriban watu 1,200 wakiuawa.
Inakadiriwa takriban 56,647 wameuawa huko Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas.
Haijabainika mara moja iwapo Hamas itakubali masharti ya kusitisha mapigano.
Tangazo la Trump linakuja kabla ya mkutano na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu uliopangwa kufanyika wiki ijayo, rais huyo wa Marekani amesema atakuwa "atakuwa na msimamo thabiti".
Rais wa Marekani amesema Jumanne kwamba anaamini Netanyahu anataka kumaliza uhasama huko Gaza.
Chanzo: BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED