Mkurugenzi wa Itikadi, Mafunzo na Oganizesheni wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), amemkosoa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akisema kwamba tatizo la uhaba wa Maofisa ugani haliwezi kutatuliwa kwa wakulima kwa kuwatafuta mtandaoni.
Amesema tatizo la maofisa ugani lililopo ni kwa sababu serikali haijatenga bajeti ya kutosha ya kuajiri maofisa ugani hao.
"Bashe alizindua mpango wa utafutaji wa Maofisa Ugani kwa njia ya mtandao, akawaambia wakulima wawe wanawatafuta huko wanapowahitaji, nimwambie kwamba, tatizo siyo kuwatafuta mtandaoni, shida iliyopo ni kwamba, hawatoshi ni wa kuongeza.
"Sisi CHAUMMA tutaweka bajeti ya kutosha ya kunyanyua kilimo tofuti na ile ya Sh.trilioni 1.2 inayotengwa na serikali ya CCM, hiyo inayotengwa sasa ni ndogo sana ndio maana inasababisha washindwe kuajiri maofisa ugani wa kutosha.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED