Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Benki ya Ushirika Tanzania Aprili 28, 2025 jijini Dodoma itakayotanguliwa na kongamano la kitaifa la wanaushirika litakalojadili fursa na changamoto za uwekezaji kwenye sekta ya ushirika ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuondoa umaskini.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini humo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema kabla ya uzinduzi wa benki hiyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho kutwa atafungua kongamano hilo.
Amesema viongozi wa kitaifa, wadau wa ushirika kutoka ndani na nje ya nchi, wafanyabiashara na wananchi wa kawaida zaidi ya 5,000 watahudhuria uzinduzi huo utakaoambata na maonesho ya ushirika.
Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki kwen ye uzinduzi huo ambao ni mwanzo wa enzi mpya ya kifedha kwa wananchi kupitia benki wanayomiliki wenyewe.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo (Coop Bank). Godfrey Ng’urah, amesema benki hiyo inaanza ikiwa na mtaji wa Sh.Bilioni 58 na inamilikiwa kwa asilimia 51 na wanaushirika.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED