Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Samia Suluhu Hassan, ameahidi wananchi wa Mkoa wa Mbeya kuwa, endapo atapata ridhaa nyingine kuongoza nchi, kukamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa yaliyoko katika eneo Utengule mkoani humo.
Samia ametoa ahadi hizo leo Septemba 4, 2025, katika mkutano wa kampeni wa CCM wilayani Mbalali, mkoani Mbeya.
Dk. Samia ametoa wito kwa wafugaji kuendelea kushiriki katika kampeni ya chanjo ya mifugo na utambuzi wa mifugo yao inayoendelea nchi nzima, ili kuzalisha nyama yenye viwango vya kimataifa ambayo ina soko kubwa kimataifa.
Amewaeleza kuwa huko nyuma walikuwa wanakosa soko kwa sababu walikuwa hawana rekodi na hawachanjwi.
Amesema wameanzisha huduma ya kuchanja na kuwatambua kwa kuwa soko la nyama nje ya nchi ni kubwa, akiwataka waendelee kufuga, ili wauze nyama na wanyama hai nje.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED