Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuwa mwezi huu vituo vya kununua mahindi kufunguliwa.
Ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Mlowo, Songwe,akiwa njiani kuelekea Mbalizi, mkoani Mbeya, kwa ajili ya mkutano wa kampeni wa chama hicho.
Samia amesema anafahamu mwaka huu mahindi yamezalishwa mengi, ambapo bado mkoani humo hawajaanza kununua.
Ameahidi vituo vya kununua mahindi hayo vitafunguliwa mwezi huu (Septemba).
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED